Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 08, 2025 Local time: 19:48

Algeria imetia saini mikataba ya mafuta na Ufaransa ya dola milioni 740


Mfano wa viwanda vya nishati na mafuta nchini Algeria. Dec. 14, 2008.
Mfano wa viwanda vya nishati na mafuta nchini Algeria. Dec. 14, 2008.

Mikataba hiyo inajumuisha mikataba ya hydrocarbon kuhusu unyonyaji wa TFT (Tin Fouye-Tabankort) II na viwanda vya TFT South katika jangwa kusini mashariki mwa Algeria, pamoja na mikataba ya gesi ya asili na nishati mbadala

Kampuni ya mafuta ya serikali ya Algeria, Sonatrach ilitia saini mikataba Jumapili yenye thamani ya dola milioni 740 na kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa ya TotalEnergies, Sonatrach imesema katika taarifa yake.

Mikataba hiyo inajumuisha mikataba ya hydrocarbon kuhusu unyonyaji wa TFT (Tin Fouye-Tabankort) II na viwanda vya TFT South katika jangwa kusini mashariki mwa Algeria, pamoja na mikataba ya gesi ya asili na nishati mbadala. Mkataba wa TFT II unatoa uwekezaji wa maendeleo wa karibu dola milioni 332, na kuwezesha kupata mita za ujazo bilioni 43 za gesi, tani milioni 4.3 za kemikali za gesi na tani milioni 5.7 za LPG, ilisema taarifa hiyo.

Uwekezaji wa maendeleo wa mkataba wa pili, TFT Sud, unakadiriwa kuwa dola milioni 407, na uwezekano wa kupata mita za ujazo bilioni 11.5 za gesi, tani milioni 1.3 za kemikali za gesi na tani milioni 1.6 za LPG iliongeza. Kulingana na Sonatrach, uzalishaji wa pamoja wa mizunguko miwili ya TFT II na TFT South utazidi mapipa 100,000 ya mafuta kwa siku ifikapo mwaka 2026 dhidi ya uzalishaji wa sasa wa mapipa 60,000 ya mafuta kwa siku.

Forum

XS
SM
MD
LG