Kiongozi huyo msitaafu alifariki dunia Mei 12, 2023 katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam, alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.
Rais Samia na viongozi mbalimbali wakishiriki kuuwaga mwili wa hayati Membe
Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi mbalimbali wameshiriki Jumapili katika Viwanja vya Karimjee mjini Dar es Salaam kuuwaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, hayati Bernard Membe, katika awamu ya nne, ya Rais msitaafu Jakaya Kikwete.

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam

2
Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili katika viwanja vya Karimjee Dar es saalam kuwaongoza Watanzania kuuaga mwili wa hayati Bernard Membe.

3
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakiwa ni miongoni mwa Watanzania waliofika kutoa heshima yao ya Mwisho viwanja vya Karimjee.

4
Gari lililo ubebea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe likiwasili katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es saalam.