Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 06:45

Rais Biden amuenzi Martin Luther King Jr. katika ibada maalum Atlanta


Rais Biden amuenzi Martin Luther King Jr. katika ibada maalum Atlanta
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:49 0:00

Rais Joe Biden amefanya ziara ya kihistoria Jumapili katika “kanisa la uhuru Marekani” kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Martin Luther King Jr., akisema demokrasia ilikuwa katika kipindi cha hatari na kwamba maisha na urithi wa kiongozi wa haki za kiraia “yanatuonyesha njia na tuendelee kuzingatia.”

Akiwa rais wa kwanza aliyeko madarakani kutoa hotuba ya kiroho Jumapili asubuhi katika Kanisa la Kibaptist la Ebenezer, Atlanta, Biden alielezea swali linalojieleza kuwa King yeye mwenyewe aliwahi kuliuliza taifa. “Alisema, “Wapi tunaelekea kutoka hapa tulipo?” Biden alisema akiwa katika membari. “Basi, ujumbe wangu kwa taifa hili katika siku hii uwe tunasonga mbele, tunakwenda pamoja, tunapochagua demokrasia dhidi ya udikteta,

jamii yenye upendo dhidi ya ghasia, tunapochagua waumini na ndoto hizo maalum, ili tuwe watendaji, kutokuwa na uoga, tukishikamane katika imani.”

XS
SM
MD
LG