Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:07

Biden na Harris kukutana na familia ya Martin Luther King Jr. miaka 60 ya matembezi ya Washington


Kundi kubwa la watu limekusanyika kushuhudia sherehe za kuweka maua katika sanamu la kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. katika siku ya maadhimisho ya Martin Luther King Jr, Washington, Jan. 16, 2023.
Kundi kubwa la watu limekusanyika kushuhudia sherehe za kuweka maua katika sanamu la kumbukumbu ya Martin Luther King Jr. katika siku ya maadhimisho ya Martin Luther King Jr, Washington, Jan. 16, 2023.

Watoto wote wa King wamealikwa, maafisa wa White House wameeleza.

Rais Mdemokrat alikuwa anaweka historia kwa kufungua ofisi ya rais maarufu ‘Oval Office’ kwa familia ya King. Mnamo mwezi Agosti 28, 1963, siku ambayo matembezi ya Washington kwa ajili ya Ajira na Uhuru, Rais John F. Kennedy alimkaribisha King na waandaaji wengine wakuu wa matembezi hayo katika ofisi ya Oval kwa mkutano.

White House haikujumuisha ratiba ya mkutano wa Biden kwa shughuli zake za umma siku ya Jumatatu.

Rais Joe Biden na Makamu wake Kamala Harris
Rais Joe Biden na Makamu wake Kamala Harris

Biden pia atakuwa mwenyeji wa hafla ya Jumatatu jioni ya maadhimisho ya miaka 60 ya Kamati ya Mawakili kwa Haki za Kiraia Chini ya Sheria, taasisi ya kisheria isiyofungamana na upande wowote wa siasa na siyo ya kibiashara ambayo ilianzishwa kwa ombi la Kennedy kwa ajili ya kuhamasisha usawa wa rangi.

Matembezi ya mwaka 1963 yanachukuliwa kuwa ni moja ya maandamano makubwa kabisa yaliyoleta matokeo muhimu zaidi ya usawa wa rangi katika historia ya Marekani.

Maandamano hayo yaliyokuwa hayana ghasia yaliwavutia takriban watu 250,000 katika viwanja vya Lincoln Memorial na kutoa chachu kwa bunge la Marekani kupitisha sheria ya kihistoria ya haki za kiraia na haki ya kupiga kura katika miaka iliyofuatia. King aliuawa mwezi Aprili 1968 huko Memphis, Tennessee.

Siku ya Jumamosi, maelfu walikusanyika katika viwanja vya National Mall kwa ajili ya kumbukumbu ya matembezi hayo, huku wazungumzaji na wengine wakisema nchi bado inakabiliwa na ubaguzi wa rangi bado haijaweza kutimiza ndoto ya King ya jamii isiyokuwa na ubaguzi wa rangi ambapo watoto wake wanne “ hawataangaliwa kwa sababu ya rangi yao ya ngozi lakini watathaminiwa kwa mwenendo wa tabia zao.”

Tukio hilo liliandaliwa na Taasisi ya Drum Major Institute ya familia ya King na Mtandao wa Al Sharpton wa National Action.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

Forum

XS
SM
MD
LG