Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 20:07

Marekani: Biden ashiriki katika ibada ya kumuenzi Martin Luther King Jr. Atlanta


Seneta Raphael Warnock, Mdemokrat akimkaribisha Rais Joe Biden kuhutubia katika kanisa la Kibaptist la Ebenezer Atlanta, Jan. 15, 2023, katika maadhimisho ya hayati Martin Luther King Jr.
Seneta Raphael Warnock, Mdemokrat akimkaribisha Rais Joe Biden kuhutubia katika kanisa la Kibaptist la Ebenezer Atlanta, Jan. 15, 2023, katika maadhimisho ya hayati Martin Luther King Jr.

Rais Joe Biden amefanya ziara ya kihistoria Jumapili katika “kanisa la uhuru Marekani” kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Martin Luther King Jr., akisema demokrasia ilikuwa katika kipindi cha hatari na kwamba maisha na urithi wa kiongozi wa haki za kiraia “yanatuonyesha njia na tuendelee kuzingatia.”

Akiwa rais wa kwanza aliyeko madarakani kutoa hotuba ya kiroho Jumapili asubuhi katika Kanisa la Kibaptist la Ebenezer, Biden alielezea swali linalojieleza kuwa King yeye mwenyewe aliwahi kuliuliza taifa.

“Alisema, “Wapi tunaelekea kutoka hapa tulipo?” Biden alisema akiwa katika membari. “Basi, ujumbe wangu kwa taifa hili katika siku hii uwe tunasonga mbele, tunakwenda pamoja, tunapochagua demokrasia dhidi ya udikteta, jamii yenye upendo dhidi ya ghasia, tunapochagua waumini na ndoto hizo maalum, ili tuwe watendaji, kutokuwa na uoga, tukishikamane katika imani.”

Katika nchi ambayo iliyogawanyika baada ya miaka miwili tu ya kuondokana na mapinduzi yenye ghasia, Biden aliwaeleza waumini, maafisa waliochaguliwa na viongozi mbalimbali kuwa: mapambano kwa ajili ya kuimarisha roho ya taifa hili ni suala la kudumu. Ni juhudi endelevu … kati ya matumaini na hofu, ukarimu na ukatili, haki na ukosefu wa haki.”

Rais wa Marekani Joe Biden, katikati, akijumuika na Seneta Raphael Warnock, na Keisha Lance Bottoms, mshauri mwandamizi wa Rais Biden katika masuala ya umma, baada ya Biden kuhutubia katika kanisa la Ebenezer Baptist Church huko Atlanta, Jan. 15, 2023 katika ibada ya kumuenzi mtetezi wa haki za kiraia hayati Martin Luther King Jr. (AP Photo/Carolyn Kaster)
Rais wa Marekani Joe Biden, katikati, akijumuika na Seneta Raphael Warnock, na Keisha Lance Bottoms, mshauri mwandamizi wa Rais Biden katika masuala ya umma, baada ya Biden kuhutubia katika kanisa la Ebenezer Baptist Church huko Atlanta, Jan. 15, 2023 katika ibada ya kumuenzi mtetezi wa haki za kiraia hayati Martin Luther King Jr. (AP Photo/Carolyn Kaster)

Rais Biden alizungumzia dhidi ya wale “wanaoeneza ubaguzi, misimamo mikali, mapinduzi” na alisema juhudi za kulinda demokrasia zinaendelea katika mahakama na masanduku ya kura, maandamano na njia nyingine. “Tunapata mafanikio, ahadi ya Marekani inashinda. … Lakini sihitaji kuwaambia kuwa siyo kwamba siku zote tunafanikiwa. Tunaweza kuporomoka. Tunafeli na kuanguka.”

Kuhudhuria kwake katika Kanisa la Ebenezer kumetokea wakati nyeti kabisa kwa Biden baada ya Mwanasheria Mkuu Merrick Garland Alhamisi kutangaza kuteuliwa kwa mwanasheria maalum kuchunguza namna rais alivyoshughulikia nyaraka za siri baada ya kuondoka katika wadhifa wa makamu wa rais mwaka 2017. White House Jumamosi iliweka bayana kuwa nyaraka zaidi za siri ziligundulika katika nyumba ya Biden karibu na mji wa Wilmington, Delaware.

Wakati akimtambulisha Biden, mchungaji mkuu wa kanisa hilo, Seneta Mdemokrat, Raphael Warnock alieleza kuwa rais ni “mkatoliki mcha mungu” ambaye “ibada hii ya Kibaptist inaweza kuwa imechangamka na ina sauti ya juu. Lakini nilimuona akiwa ameketi anapiga makofi.”

King, “mhubiri mashuhuri kabisa wa Marekani wa karne ya 20,” kama alivyoiweka Warnock, alihudumu kama mchungaji mwenza kutoka 1960 mpaka alipouawa mwaka 1968.

Warnock, kama ilivyokuwa kwa Wademokrat wengi kwenye majimbo yaliyokuwa na ushindani mkali walioshinda kwa mara nyingine tena uchaguzi 2022, alikaa mbali na Biden wakati wa kampeni ilipokuwa Biden uungawaji mkono wa urais wake ulishuka na mfumuko wa bei ukiongezeka.

Lakini baada ya uchaguzi kumalizika na akiwa na kipindi cha miaka sita ya uongozi mbele yake, Warnock alimkaribisha kikamilifu Biden katika ibada kwenye kanisa lake. Kabla ya kumalizika ibada hiyo, alimtaka Biden aende mbele ya kanisa hilo na kuwataka waumini wa kanisa la Ebenezer kumuombea rais wakati akiorodhesha mafanikio kadhaa ya kisheria ya Biden.

“Hilo, marafiki zangu, ni kazi ya Mungu,” alisema Warnock, akiongeza kuwa Biden “alikuwa ana mchango wa kiasi fulani katika hilo.”

Wakati Biden akianza kuangazia kwenye matarajio ya juhudi za kuchaguliwa tena 2024, ataendelea kuangaza zaidi huko Georgia.

Mwaka 2020, Biden alifanikiwa kushinda Georgia na pia alipata ushindani Michigan na Pennsylvania, ambako wapiga kura Weusi walikuwa na ushiriki wenye uwiano mdogo kati ya wapiga kura Wademokrat. Kuwaleta wapiga kura Weusi katika majimbo hayo itakuwa ni muhimu kwa matumaini ya ushindi wa Biden 2024.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG