Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 12:06

Mawakili wa familia ya Patrick Lyoya, kutoa matokeo ya uchunguzi huru wa maiti Jumanne.


Polisi wa Grand Rapids na Wyoming wakipambana na waandamanaji waliokuwa wakipinga mauaji ya Patrick Lyoya mjini Michigan
Polisi wa Grand Rapids na Wyoming wakipambana na waandamanaji waliokuwa wakipinga mauaji ya Patrick Lyoya mjini Michigan

Mawakili wa familia ya Patrick Lyoya, mtu Mweusi ambaye hakuwa na silaha aliyeuawa na polisi magharibi mwa Michigan, walisema watatoa matokeo ya uchunguzi huru wa maiti leo  Jumanne.

Video kutoka kwa mpita njia inaonyesha Lyoya akiwa chini alipopigwa risasi ya kichwa wakati wa mvutano na afisa mzungu wa Grand Rapids siku ya Aprili 4. Ripoti rasmi ya uchunguzi wa maiti inawasilishwa polisi na haitatolewa mara moja kwa umma.

Lakini uchunguzi tofauti wa maiti uliofanywa na Dk. Werner Spitz, mtaalamu wa uchunguzi wa maiti mwenye umri wa miaka 95 ambaye alifanya kazi katika uchunguzi kufuatia mauaji ya Rais John F. Kennedy na Martin Luther King Jr., miongoni mwa kesi nyingine maarufu. Yeye ni mkaguzi wa zamani wa maiti katika eneo la Detroit.

Kifo cha Lyoya kimeikasirisha familia yake pamoja na watu wengi ambao wametazama video ya makabiliano yake na afisa mmoja wa Polisi.

Polisi huyo ambaye jina lake halijatangazwa, anasikika akisema kuwa nambari ya gari si ya gari hilo. Lyoya alikataa kurejea ndani ya gari kama alivyoamriwa, na wakaanza kufukuzana.

Katika dakika za mwisho, afisa huyo alikuwa juu ya Lyoya, akijaribu kumzuia. Alifyatua bunduki yake baada ya kumtaka Lyoya aache kifaa chake cha umeme -Taser ya polisi.

Lyoya ni mkimbizi kutoka Congo na anatarajiwa kuzikwa Ijumaa na mtandao wa Kitaifa wa mchungaji Al Sharpton ulisema utasaidia kulipia gharama. Na mchungaji huyo atatoa wasifu wa marehemu katika ibada.

XS
SM
MD
LG