Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 09:35

Qatar yaonya 'hatari kuongezeka' baada ya Marekani na Uingereza kulipiza kisasi


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar kwenye mkutano wa waandishi wa habari Qatar.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar kwenye mkutano wa waandishi wa habari Qatar.

Mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Uingereza hayatazuia mashambulizi ya wa- Houthi wa Yemen kwenye njia za meli za kibiashara katika Bahari ya Sham bila juhudi za kidiplomasia.

Kauli hiyo ameitoa Waziri Mkuu wa Qatar Jumanne wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi la Dunia, WEF, huko Davos.

Sheikh Mohammed Bin Abdulrahman al- Thani amesema Qatar inaamini kwamba kupunguza mzozo huko Gaza kunaweza kusimamisha kuenea kwingineko.

Aliongeza kuwa hali ya sasa katika eneo ni kichocheo cha kuenea katika maeneo mengine.

Waziri mkuu wa Qatar na mambo ya nje sheikh Mohammed bin Abdulrahman alisema:

“ Sasa tunaona kuna kujibu mashambulizi kutoka Marekani na Uingereza dhidi ya Wa- Houthi, wakijaribu kuwazuiya kuvuruga biashara ya kimataifa.

lakini hili pia litasababisha hatari kubwa na kuenea zaidi. Siku zote tunajali zaidi diplomasia katika suluhu yoyote ya kijeshi na tunaamini kwamba tusizingatie sana mizozo midogo. Tulenge mzozo mkubwa. Na mara utakapoondolewa naamini kila kitu kitaondolewa."

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG