Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 21:00

Wahouthi wanaonekana kupuuzia maonyo ya Marekani


Wanamgambo wa Kihouthi wanaonekana kupuuza maonyo ya Marekani, kwa mashambulizi yao ya mara kwa mara dhidi ya meli katika bahari ya Sham.

Wanamgambo hao walipeleka boti isiyo na nadhodha Alhamisi ambayo ilikaribia umbali mdogo kutoka meli za kibiashara na kivita za Marekani kabla ya kulipuka.

Maafisa wa jeshi la majini la Marekani wamesema meli hiyo iliyoendeshwa kutoka eneo la Wahouthi wa Yemen na kufika takriban maili 50 kwenye njia ya meli zenye shughuli nyingi kabla ya kulipuka.

Wamesema haijulikani ni nani au ni nini Wahouthi walijaribu kukilenga, na kuongeza kuwa mlipuko huo haukusababisha uharibifu wowote au madhara kwa watu.

“Hakuna dalili kwamba wataacha kile wanachokifanya,” amesema kamanda Brad Cooper, mkuu wa operesheni za Jeshi la Wanamaji la Marekani kwa Mashariki ya Kati.

Forum

XS
SM
MD
LG