Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 17:02

Polisi wawatawanya waalimu Morocco wakipinga mikataba ya ajira


Maelfu ya wananchi wa Morocco wakishiriki katika maandamano nchini humo kupinga kukamatwa kwa wanaharakati waliokuwa wakiandamana huko Rabat, Morocco, Jumapili, Aprili 21, 2019.
Maelfu ya wananchi wa Morocco wakishiriki katika maandamano nchini humo kupinga kukamatwa kwa wanaharakati waliokuwa wakiandamana huko Rabat, Morocco, Jumapili, Aprili 21, 2019.

Zaidi ya waandamanaji 70 wamejeruhiwa baada ya polisi katika mji mkuu wa Morocco, wa Rabat, wakitumia maji yanayotoka kwa kasi kutawanya mkusanyiko wa maelfu ya walimu waliokuwa wakiandamana, wakilalamika dhidi ya kanuni za mikataba yao ya kuajiriwa.

Walimu waliopaaza sauti zenye ujumbe wa kutaka haki ya kijamii, na kupinga uongozi mbovu katika shule za uma, walijaribu kupiga kambi nje ya bunge la taifa, katikati mwa Rabat, wakitaka matakwa yao kushughulikiwa, lakini polisi walitumia nguvu kuvunja maandamano hayo.

Walimu katika shule za uma, wakiwa wamevalia koti nyeupe, walitoka miji tofauti kote nchini kwa maandamano hayo, baada ya mkutano uliokuwa umepangiwa baina yao na maafisa wa wizara ya elimu kuahirishwa siku ya Jumanne.

Zaidi ya walimu 55,000 walioajiriwa kwa kandarasi za muda mwaka 2016, walianzisha mgomo mwezi Machi mwaka 2019 na kufanya maandamano makubwa ili kuhimiza matakwa yao yatekelezwe ya kuajiriwa kwa mikataba ya kudumu ili kuboresha hali yao hasa watakapostaafu.

Walimu wanaofanya kazi kwa mkataba wa mda mfupi nchini Morocco wanalipwa dola 520, sawa na wenzao walioajiriwa kwa mkataba wa kudumu, lakini hawapokei marupurupu yoyote, ikiwemo malipo ya pensheni.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG