Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 04:44

Algeria : Polisi wawakamata waandamanaji wanaopinga Bouteflika kugombea urais awamu ya tano


Abdelaziz Bouteflika
Abdelaziz Bouteflika

Polisi wa Algeria wamewakamata baadhi ya waandamanaji mjini Algiers Jumapili baada ya maandamano kuendelea siku tatu mfululizo.

Wananchi wa Algeria walijitokeza katika maandamano ambayo nadra kufanyika nchini humo kupinga mipango ya kuongeza muda wa utawala wa rais asiyeonekana Abdelazizi Bouteflika kwa mhula wake wa tano.

Makundi ya watu walijitokeza mitaani katika mji mkuu wa Algiers na miji mingine mikubwa wakiwataka maafisa wa serikali kutupilia mbali mipango ya kumtaka rais Butelflika mwenye umri wa miaka 81 kugombea nafasi ya urais baada ya miaka 20 ya utawala ifikapo Aprili 8.

Buteflika aliyeko madarakani tangu 1999 alipatwa na kiharusi 2013 na tangu wakati huo ni mgonjwa na haonekani hadharani mara nyingi.

Wapinzani wake wanadai kwamba hakuna ushahidi unaothibitisha kwamba yuko katika hali nzuri ya kiafya kuweza kuiongoza nchi hiyo wakisema inaongozwa na washauri wake.

Tangu chama tawala cha FLN kumteua Buteflika kuwa mgombea wa urais vyama kadhaa vya kisiasa, vyama vya wafanyakazi na mashirika ya kibiashara yamesema yatamuunga mkono.

Upinzani unakabiliwa na vizingiti vingi kuweza kuleta ushindani katika uchaguzi. Vikosi vya usalama vimeweza kukandamiza malalamiko ya waandamanaji wa Algeria hata wakati wa wimbi la mapinduzi ya nchi za kiarabu mwaka 2011.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG