Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 03:13

Polisi : Shambulizi la Australia lahusishwa na ugaidi


Kikosi cha waokoaji kikiwa karibu na mtaa wa biashara wa Bourke Melbourne, Australia, Novemba 9, 2018.

Mtu mmoja amewashambulia kwa kisu watu kadhaa, na kumuuwa mtu mmoja katika mji wa Melbourne Ijumaa.

Polisi wa Australia wamesema wanaamini kuwa shambulizi hilo la Melbourne, mji wa pili kwa ukubwa katika nchi hiyo, linahusishwa na ugaidi.

Kikosi cha kupambana na ugaidi kinaongoza uchunguzi huo, serikali imeeleza.

Kamishna wa polisi wa jimbo la Victoria Graham Ashton amesema mshukiwa huyo ambaye aliuwawa, ni mwenye asili ya Kisomali na alikuwa anafuatiliwa na polisi.

Polisi walimrushia risasi mshukiwa huyo wakati alipokuwa anawaonyesha kisu maafisa wa polisi wawili katikati ya eneo la jiji hilo, kabla ya afisa mmoja kumpiga risasi kifuani. Alipelekwa hospitali na baadae kufariki.

Hapo awali polisi waliitikia wito wa taarifa ya gari lililokuwa linaungua, lakini walipowasili katika eneo la tukio walikuta watu wamepigwa visu.

Mshukiwa huyo alikuwa anaendesha gari lililokuwa limebeba mitungi ya gesi katika mtaa huo wa tukio, ambapo tukio hatarishi, lakini sio la kigaidi lilitokea mwezi Januari 2017 ambapo mtu mmoja alitumia gari yake kuwashambulia wanaotembea kwa miguu, na kuuwa watu sita na kujeruhi 30.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG