Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 22:21

Polisi Nigeria wakubali kutotumia tena nguvu dhidi ya waandamanaji


Waandamanaji wanataka kikosi maalum cha kupambana na wizi SARS kuvunjwa wakiwa kwenye kituo cha kulipa ushuru wa magari Lagos, Nigeria, Oct. 12, 2020.
Waandamanaji wanataka kikosi maalum cha kupambana na wizi SARS kuvunjwa wakiwa kwenye kituo cha kulipa ushuru wa magari Lagos, Nigeria, Oct. 12, 2020.

Polisi wa Nigeria wamekubali kutotumia tena nguvu dhidi ya waandamanaji siku moja baada ya polisi kutumia risasi na kuwauwa waandamanaji wawili mjini Logos.

Wakati huo huo waandamanaji wamekasirishwa na uamuzi wa mkuu wa polisi Mohammed Adamu kutangaza Jumanne kwamba wanaunda kikosi kipya maalum kuchukua nafasi ya kikosi maalum cha kupambana na wizi, SARS, kilichovunjwa Jumapili.

Mageuzi katika Kikosi cha Polisi.

Kwa wiki moja sasa vijana wa Nigeria wamekua wakiandamana katika miji mbalimbali ya taifa hilo lenye wakazi wengi kabisa barani Afrika wakilalamika dhidi ya mateso na ukatili na mauaji yanayofanywa na polisi wakidai mageuzi juu ya namna polisi inavofanya kazi.

Waandamanaji hawajaridhika na uamuzi wa mkuu wa polisi Adamu kutangaza kuundwa kwa kikosi maalum cha silaha na mbinu SWAT kuchukua nafasi ya SARS.

Wasani mashuhuri wa nchi hiyi wameungana na wananchi kudai mageuzi. Mmoja wa wasanii hao DX2 anasema : "Ni mambo mengi tu, sio tatizo la SARS tena. Kuna njaa hapa nchini, uchumi ni mbaya, hakuna hata taa, barabara ni tatizo, hakuna maji pia. Uhalifu umeongezekla huko kaskazini, utekaji nyara na wanamgambo wanaopigana kaskazini. Kwani tulikuchagua ufanye nini? Tulikuchagua utulete mageuzi."

Wanaharakti wa Nigeria na mashirika ya kutetea haki za binadamu ya kimataifa wanakilaumu kikosi cha SARS kwa unyanyasaji, mateso na mauaji ya raia.

Amnesty International ilieleza Jumanne kwamba watu 10 wameuliwa mnamo maandamano ya wiki nzima sasa.

Kalu Kingsley alilazimika kukatwa mguu baada ya kupigwa kwa risasi na polisi wa SARS mwezi oktoba 2017. Maafisa wa polisi walisema ilikuwa ni ajali aipopigwa risasi na polisi aliyetuhumiwa aliendelea kufanya kazi huku Kingsley akitumia maelfu ya dola kupata matibabu bila ya kulipwa fidia.

Kingsley anaeleza : Ikiwa ameweza kusababisha kiwango hichi cha majeraha kwangu mimi na bila ya kuchukuliwa hatua, basi mmempatia nguvu ya kutenda mambo mabaya zaidi. Na umewapatia wenzake nguvu pia."

Masuala kuhusu ukatili unaofanywa na polisi wa SARS yamekuwa yakiendelea kwa miaka kadhaa huko Nigeria.

Buhari akivunja kikosi cha SARS

Siku ya Jumapili Rais Muhammadu Buhari aliitikia wito wa waandamanaji na kukivunja kikosi hicho na kuahidi mageuzi kamili ya polisi.

Lakini waandamanaji wengi hawajakubaliana na tangazo hilo kwani polsi waliokuwa kwenye kikosi hicho watapewa mafunzo na kupelekwa katika vikosi vingine jambo linalopingwa na waadamanaji wanaosema wataendelea kuandamana hadi mageuzi kamili yafanyike.

Muimbaji wa Rap Cobany anasema ni mtizamo kamili wa polisi unabidi kubadilika.

Cobany muathiriwa wa ukatili wa polisi anaeleza : "Ni zaidi ya kuwazuia au kuvunja kikosi kamili au kuwapiga marufuku. Ni suala la kisaikolojia, mtizamo na mawazo yao yanabidi kubadilishwa.

Mkurugenzi wa kitaifa wa Amnesty International Osai Ojigho anasema kuvunjwa kikosi haitoshi bila ya kuwalipa fidia waathiriwa.

Maafisa wa Nigeria wameahidi kuunda kamati ya ushauri itakayongozwa na raia kusimamia utaratibu wa mageuzi ya kikosi cha polisi.

XS
SM
MD
LG