Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:24

Licha ya janga la Covid makundi ya kigaidi yaendelea na harakati za kuimarisha ngome zao-AFRICOM


Nembo ya kikosi cha Marekani kwa jailli ya Afrika-AFRICOM.
Nembo ya kikosi cha Marekani kwa jailli ya Afrika-AFRICOM.

Makundi ya kigaidi yenye itikadi kali maarufu VEOS yanatumia kipindi hiki kigumu cha janga la Corona, kwa kuendelea na harakati zao hasa katika jamii zinazokumbwa na janga hilo, kuanzia huko Msumbiji hadi Nigeria, kamanda wa operesheni maalum za jeshi la Marekani barani Afrika, Major Gen Dagvin Anderson amesema.

Kamanda huyo alizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao kutoka makao makuu ya kikosi cha jeshi la Marekani kwa ajili ya afrika AFRICOM makundi ya kigaidi yanaendelea na harakati za kuimarisha ngome zao,M mjini Stuttgart, Ujerumani.

Katika kanda ya Afrika magharibi, wanaharakati wenye itikadi kali ya kiislamu walivuruga mifumo ya elimu. Kamanda Anderson ametaja zaidi ya shule elfu tatu zilizoharibiwa na makundi ya wanaharakati hao nchini Mali na Burkina Faso.

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya kati na Msumbiji wametumia malalamiko ya wakazi kutokana na maisha magumu ili kuendelea na harakati zao.

Anderson anasema, baadhi ya makundi hayo ya kigaidi yanategemea msaada wa nje kutoka makundi ya mamluki.

Kundi la mamluki lenye uhusiano na Russia maarufu Wagner Group, linadhaniwa kufanya harakati nyingi katika nchi 20 za Afrika zikiwemo Msumbiji, Libya, Sudan, Ivory Coast na Jamuhuri ya Afrika ya kati.

Anderson anakubaliana na wachambuzi wanaoamini kuwa kundi la Wagner lina mahusiano na Kremlin, madai yanayopingwa na Russia.

Anderson amegusia pia taarifa ya hivi karibuni kwamba makao maku ya AFRICOM, yatahamishwa kutoka ujerumani kuelekea nchi moja wapo ya ulaya.

Amesisitiza kuwa matatizo yaliosababishwa na janga la virusi vya corona hayatabadili chochote wala kupunguza operesheni za jeshi la Marekani barani Afrika, na kueleza kuwa kubadili makao makuu hakutokua na athari kubwa kwenye shughuli zao.

Kinachomtia wasi wasi, ni athari mbaya za janga la corona kwenye huduma za serikali na taasisi za Afrika. Ameonya pia kwamba jukumu la jeshi lina mipaka, mara nyingi jeshi huingilia kati kwa kuchelewa.

Suluhisho la jeshi peke yake halitaweza kutatua mahitaji yao ya usalama wa chakula, shule, huduma bora za afya na huduma za kimsingi za serikali.

Baadhi ya makundi hayo ya kigaidi yanadai kuwa yamekuja kumaliza ukosefu huo wa haki, lakini Anderson anasema kuwa njia zao za dhulma zitafikia kikomo.

XS
SM
MD
LG