Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:50

Polisi Israeli wamuua mshambuliaji mwenye silaha huko Old Jerusalem

Wanausalama na kikosi cha uokozi cha Zaka wamembeba mwanaume wa Kipalestina aliyeuawa na polisi wa Israeli baada ya kumuua Israeli mmoja and na kuwajeruhi wengine wanne katika mji wa Old City, Jerusalem Jumapili, Nov. 21, 2021. (AP Photo/Mahmoud Illean)

Maafisa wanasema mwanaume wa Kipalestina ameuawa kwa kupigwa risasi na majeshi ya Israeli baada ya kuwafyatulia risasi na kuwajeruhi watu wanne Jumapili katika mji wa Old City, huko Jerusalem.

Kwa mujibu wa Haaretz, maafisa wa Israel wamemtambua mwanamme huyo aliyefyatua risasi kuwa ni Fadi Abu Shehadam, umri miaka 42, kutoka Jerusalem Mashariki “anaye julikana kuwa na mahusiano na kikundi cha Hamas.”

Tukio hilo lilitokea katika eneo maarufu ambalo ni takatifu kwa wote Wayahudi na Waislam. Linajulikana na Wayahudi kama Temple Mount na Waislam kama Noble Sanctuary.

Maafisa wa Israeli wanasema mmoja wa wale waliopigwa risasi na mshambuliaji huyo baadae alifariki kutokana na majeraha.

Shambulizi hilo la Jumapili ni la pili katika siku za karibuni. Kijana mmoja aliuawa Jumatano huko Old City baada ya kuwachoma visu maafisa wawili wa polisi wa mpakani.

Baadhi ya habari katika ripoti hii zinatokana na vyanzo vya habari vya AP na Reuters.

XS
SM
MD
LG