Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 18, 2025 Local time: 03:14

Patrick Zaki atoka gerezani


Picha ya Patrick Zaki kutoka ukurasa wa Facebook Julai 20, 2023, baada ya kuachiliwa kutoka kizuizini huko Mansoura. Picha na "Patrick Libero" ukurasa wa Facebook / AFP.
Picha ya Patrick Zaki kutoka ukurasa wa Facebook Julai 20, 2023, baada ya kuachiliwa kutoka kizuizini huko Mansoura. Picha na "Patrick Libero" ukurasa wa Facebook / AFP.

Mtafiti wa Misri Patrick Zaki ametoka gerezani siku ya Alhamisi familia yake ilisema, siku moja baada ya Rais Abdel Fattah al-Sisi kumpa msamaha kufuatia kilio cha kimataifa.

Zaki siku ya Jumanne alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la "kusambaza habari za uongo" kitu ambacho kiliwachochea baadhi ya washiriki kutoka nje ya majadiliano ya serikali yenye lengo la kuwapa wapinzani sauti.

"Patrick yuko huru," dada yake, Marise George, alisema Alhamisi kupitia mtandao wa Facebook, akiambatanisha picha ya mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 32 akiwa nje ya gereza la Mansoura, lililopo takriban kilomita 110 kaskazini mwa mji mkuu Cairo.

Zaki alifungwa kutokana na nakala iliyochapishwa mwaka 2019 inayoelezea ubaguzi ambao yeye na washiriki wengine wa kikristo wa dhehebu la Coptic walio wachache nchini Misri wakisema mateso waliyoyapata.

Rais Sisi siku ya Jumatano alitoa msamaha kwa Zaki na watu wengine watano -- wanaume watatu na wanawake wawili.

Msamaha huo unamjumuisha Mohamed al-Baqer, wakili wa Alaa Abdel Fattah, mfungwa maaarufu wa kisiasa nchini Misri, kulingana na amri iliyochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG