Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 13, 2025 Local time: 06:15

Rais wa Misri amempa heshima kubwa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi


Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi (R) akipeana mkono na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi mjini Cairo. June 25, 2023.
Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi (R) akipeana mkono na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi mjini Cairo. June 25, 2023.

Viongozi hao walitia saini tamko la kuongeza uhusiano kati ya Misri na India na ushirikiano wa kimkakati, ikimaanisha kwamba mataifa hayo mawili yamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao na kufanya mazungumzo ya mara kwa mara

Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi, amempa heshima kubwa waziri mkuu wa India Narendra Modi wakati nchi hizo mbili zikiimarisha ushirikiano wao.

El-Sissi alimkaribisha Modi katika makazi ya rais mjini Cairo kwa kufuata kanuni za “Order of the Nile”, ofisi ya Rais wa Misri imesema katika taarifa. Viongozi hao walitia saini tamko la kuongeza uhusiano kati ya Misri na India na ushirikiano wa kimkakati, ikimaanisha kwamba mataifa hayo mawili yamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao na kufanya mazungumzo ya mara kwa mara.

Misri na India zina uhusiano wa kina ambao ulianza miaka ya 1950 wakati walipofanya majukumu muhimu katika kuanzisha Harakati zisizo za Kiutawala ambazo zilitafuta njia mbadala wakati wa Vita Baridi.

Modi, ambaye aliwasili Cairo Jumamosi ni Waziri Mkuu wa kwanza wa India kufanya ziara ya kitaifa nchini Misri katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili. Ziara yake ya siku mbili imekuja miezi sita baada ya el-Sissi kutembelea mjini New Delhi kama mgeni rasmi katika Siku ya Uhuru wa India.

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi pia alimwalika kiongozi huyo wa Misri kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 tajiri na zinazoendelea, ambazo India itakuwa mwenyeji wa mkutano huo mwezi Septemba.

Forum

XS
SM
MD
LG