Zaki amekuwa akisoma nchini Italy kabla kukamatwa wakati wa ziara yake nyumbani mwaka wa 2020 kutokana na makala ya uchunguzi aliofanya kuhusu hali ngumu ya maisha ya Wakristo nchini Misri.
Atarejea Italy leo Alhamisi, waziri mkuu wa Italy Giorgia Meloni amesema katika taarifa ambapo alimshukuru Sisi “kwa kitendo hicho muhimu sana.”
Msamaha wa Sisi, ambao uliripotiwa na shirika la habari la serikali na kuthibitishwa na mawakili, unamuhusu pia Mohamed El-Baqer, mwanasheria ambaye alikuwa wakili wa mwanaharakati maarufu Alaa Abdel-Fattah ambaye alikamatwa mwaka wa 2019 wakati akihudhiria mahojiano ya mteja wake.
Forum