Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 21:25

Pande mbili kinzani za kisiasa Sudan zaingia mitaani


Waandamanaji nchini Sudan wakishinikiza kuvunjwa kwa serikali ya mpira, nje ya kasri ya rais mjini Khartoum, Sudan, Jumamosi, Oktoba 16, 2021. (AP Photo/Marwan Ali)
Waandamanaji nchini Sudan wakishinikiza kuvunjwa kwa serikali ya mpira, nje ya kasri ya rais mjini Khartoum, Sudan, Jumamosi, Oktoba 16, 2021. (AP Photo/Marwan Ali)

Wafuasi wa serikali ya mpito ya Sudan wameingia mitaani kwenye mji mkuu Khartoum Alhamisi wakati waandamanaji wapinzani wanataka kurejeshwa kwa utawala wa kijeshi.

Pande zote mbili zimetoa wito kwa wafuasi wao kukaa mbali na kujizuia na ghasia zozote lakini kulikuwa na polisi wengi na wanajeshi waliozingira maeneo muhimu.

Pande mbili zinawakilisha makundi ya upinzani ya Force for freedom and change, chini ya mwamvuli wa kundi la kiraia, ambalo lilichochea maandamano ya kitaifa yaliyopelekea jeshi kumtimua kiongozi wa muda mrefu Omar Al Bashir mwaka 2019.

Kundi hilo linaunga mkono kipindi cha mpito wa kiraia wakati wafuasi wa kundi lililojitenga linataka jeshi kuchukua udhibiti.

Tangu Jumamosi kundi linalounga mkono jeshi limekuwa likiketi nje ya makazi ya rais.

Limewavuta raia wengi wa Sudan ambao wameathiriwa na mageuzi magumu yanayoungwa mkono na Shirika la Fedha Duniani - IMF yaliyotekelezwa na Waziri Mkuu Abdallah Hamdock, mchumi wa zamani wa Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG