Upatikanaji viungo

Breaking News

Pakistan : Ajali ya moto ndani ya treni yaua abiria 74


Treni ikiwaka moto baada ya mtungi wa gesi kuripuka wakati abiria walipokuwa wakipika chakula cha asubuhi karibu na mji wa Rahim Yar Khan jimbo la mashariki la Punjab , Pakistan Octoba 31, 2019,Pakistan's Punjab Emergency Service Rescue/AFP

Watu 74 waliokuwa katika treni ya abiria wamepoteza maisha baada ya mtungi wa gesi ambao abiria walikuwa wanatumia kupika chakula cha asubuhi kuripuka ndani ya treni hiyo.

Katika ajali hiyo abiria wengine kadhaa walijeruhiwa. Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Rahimyar Khan katika jimbo la mashariki la Punjab, maafisa wa Pakistan wamesema.

Picha za televijeni zimeonyesha moto mkubwa na watu walikuwa wanasikika wakilia.

Maafisa wa shirika la reli la Pakistan tayari wameanza kufanya uchunguzi juu ya tukio la ajali hiyo ya moto.

Taarifa za awali zimesema chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa mitungi miwili ya gesi iliyokuwa ndani ya treni iliyokuwa inatumiwa na abiria kupikia.

Ajali za gari moshi hutokea mara nyingi nchini Pakistan, ambako shirila la reli limeshuhudia miongo kadhaa ya kuzorota kwa uboreshwaji wa usafiri wa reli kutokana na rushwa, utawala mbovu na ukosefu wa uwekezaji.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Patrick Nduwimana, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG