Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:47

Tafiti yaonyesha ongezeko la habari feki katika uchaguzi


Mfano mtu anavyo kabiliwa na habari ambazo baadhi ni kweli na nyingine ni uongo.
Mfano mtu anavyo kabiliwa na habari ambazo baadhi ni kweli na nyingine ni uongo.

Ikiwa zimebakia siku chache tu kabla ya Wakenya kwenda kupiga kura kumchagua rais na wawakilishi wetu Agosti nane, hivi sasa kuna ongezeko la habari ambazo si za kweli.

Kundi la wataalamu liliwasilisha utafiti wao hivi karibuni kuhusiana na suala hili. Kama anavyoripoti mwandishi wa VOA Lenny Ruvaga kutoka Nairobi.

Utafiti uliofanywa na kampuni ya makampuni ya mawasiliano Portland Africa na Geo Poll ilibaini kwamba asilimia 90 ya wakenya wamekuwa wakiona au kusikia habari ambazo si za kweli kuhusu uchaguzi wa mwaka huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:36 0:00

Utafiti ulifanywa mapema mwezi Mei mwaka huu na takriban watu 2,000 kote nchini walihojiwa, walioshiriki utafiti walikuwa wa umri, jinsia, dini na makabila tofauti.

John Murunga kutoka Geo Poll anasema wakenya wengi wanaviamini vyombo vya habari kuwa ni chanzo chao kikuu cha habari za uhakika huku asilimia 76 wakisema kwamba habari zinazokusanywa na televisheni ni sahihi. Anasema kwamba kutumia vyombo mbali mbali inaweza kuwa njia ya kukabiliana na habari za uongo nchini. Hata hivyo, anaelezea kwamba zinawanyima wapiga kura habari muhimukufanya maamuzi sahihi.

“Athari za habari za uongo ni kwamba tunakuwa na watu ambao wananyimwa nguvu ya kufanya maamuzi muafaka kuhusiana na uchaguzi ujao na hiyo inaathiri nia yao, inaathiri madaraka yao kufanya maamuzi sahihi,” Anasema.

Mwezi April wakazi wa Busia, magharibi mwa Kenya waliamka wakikumbana na habari kwamba mgombea mkuu wa upinzani katika uchaguzi wa awali, Paul Otuoma wa ODM, alihamia katika ushirika wa utawala wa Jubilee.

Habari zisizo za kweli zilichapishwa kwenye vipeperushi ambavyo vilfanana na gazeti maarufu la Daily Nation nchini humo. Eneo hilo kwa kiasi kikubwa lina wafutiliaji wa upinzani.

Dorothy Ooko, meneja wa mawasialiano na masuala ya umma katika Google kwa Afrika Mashariki na nchi za Afrika zinazotumia lugha ya kifaransa, anasema wapiga kura na wenye biashara ni vyema wafahamu zipi ni habari za uongo na kubuni njia ya kukabiliana nazo.

Ooko anasema changamoto iko kwenye usahihi na kasi ambayo habari hizo zinasambazwa. Google anasema imeweka mifumo kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata habari sahihi kwenye mtandao wao kwa kuwapa habari za kweli.

“Kazi yetu kwa kweli kuwasilisha habari, kuwasilisha maeleo na kuhakikisha zinapatikana na ni zinafaa. Wao ndiyo ambao wana uwezo wa kuona na kufafanua iwapo ni ukweli au la, na halafu wawe na uwezo wa kumuongoza mtumiaji ambaye anaingia katika mtandao kuwa hilo aliliona ni la kweli. Ni ukweli kwa asilimia 80 na hivyo inakupa wewe mtumiaji, imani kwamba habari imethibitishwa na imewasaidia watu.”

Alphonce Shiundu kutoka Afrika Check, taasisi isiyo ya kiserikali na isiyoelemea upande wowote inalenga kuboresha upatikanaji wa ukweli na ukusanyaji wa habari. Amezungumza na VOA kuhusu ongezeko la mwenendo wa habari za uongo nchini Kenya. Shiundu anasema kwamba habari za uongo ni jambo liko kote ulimwenguni na vyombo vya habari vya Kenya navyo vimo halikadhalika.

“ Tunafanya ukaguzi wa ghafla kuhusu habari za uongo. Kama kuna kitu kinavuma mtandaoni tunakiangalia. Kama tukiona kitu hakijakaa sawa tunacheki na kutafuta kama ni kweli au uongo na tunaitoa habari hiyo. Tuna shirikiana na Google Facebook kusudi tunapoweka kitu mfumo unakuwa rahisi kutafuta na kufanyaukaguzi na kuangalia matokeo ya kucheki huko.”

Kwa mujibu wa ripoti ya karibuni kwa kile ambacho kipo kenye mtandao wa Akamai, Kenya iko katika nafasi ya 14 kati ya nchi 130 katika misingi ya kasi ya internet. Habari nyingi ambazo ni za uongo inasema zimechapishwa katika Facebook, Twitter na Whatsapp.

Kupanda kwa idadi ya mabloga nchini Kenya kwa mujibu wa ripoti inaonekana ni mwenendo wa kutia wasi wasi katika mapambano dhidi ya fake news. Chama cha mabloga (BAKE) ambacho kilianzishwa miaka sita iliyopita kimewaleta pamoja kiasicha wakenya 9,000 ambao ni mabloga na wamiliki wengine wa mitandao.

Mwenyekiti wa BAKE, Kennedy Kachwanya anasema taasisi yake inhakikisha kuwa wanachama wake wanaheshimu sheria kali za kutoa habari sahihi kabla ya kuzichapisha. Hata hivyo Kachwanya anasemabado kuna changamoto.

March mwaka jana Baraza la Habari Kenya (MCK), baraza hilo lina jukumu la kuhakikisha wanaheshimu taaluma kwenye vyombo vya habari Kenya, na kutoa miongozo jinsi ya kuripoti uchaguzi.

Victor Bwire, naibu mtendaji mkuuu na meneja wa mipango katika baraza hilo anasema tangu wakati kiasi cha wanahabari 2,700 wamepatiwa mafunzo jinsi ya kuandika habari sahihi na za uhakika.

Bwire anasema baraza linaushawishi umma kuviripoti vyombo vya habari ambavyo vinaripoti habari za uongo.

Ripoti inaelezea kwamba asilimia 35 ya wale waliohojkiwa wanasema hawajaweza kupata fursa na kuthibitisha ukweli wa habari zilizotolew kuhusu uchaguzi.

Wakenya watakuwa na fursa ya kupaza sauti zao kwenye vituo vya kupigia hapo Agosti 8.

XS
SM
MD
LG