Dunaini katika picha

1
Mwanamke akitembea kando ya barabara mnamo siku ambayo hewa imejaa vumbi kutokana na kuchafuka mazingira katika mji wa Changchun, jimbo la Jilin Uchina.

2
Kiongozi wa upinzani wa Burma Aung San Suu Kyi akisimama na Rais wa bunge la Ulaya Martin Schulz katika Bunge la Ulaya mjini Strasbourg, mashariki ya Ufaransa baada ya kupokea tunzo yake ya haki za binadam ya Sakharov, alotunzwa mwaka 1990 wakati wa ukandamizaji wa kijeshi huko Burma..

3
Sura inayofanana na Barack Obama na mkewe Michelle zimechongwe kwenye boga na kuashwa kwa mchuma huko Madame Tussauds, New York.

4
Kijana wa ki-Indonesian akitembea juu ya nyangumi aliyewasili pwani wakati wavuvi wanajaribu kumrudisha baharini kwenye pwani ya Kenjeran, mjini Surabaya,Java mashariki, Indonesia.