Craig Hicks alihukumiwa kutumikia kufungo cha maisha mara tatu mfululizo Jumatano kwa shtaka la kupiga bunduki ndani ya nyumba.
Hicks aliingia ghafla katika nyumba na kuwaua mwanafunzi Deah Barakat aliyekuwa anasomea udaktari wa meno na pia mkewe Yusor Abu-Salha, na dada yake Razan Abu-Salha, mnamo mwezi Februari, 2015.
Dkt Mohammad Abu-Salha, baba wa Yusor na Razan amesema : “Ulisikia namna watoto hawa walivyokuwa wazuri. Hukuonyesha majuto na kuomba msamaha au sikitiko au heshima au hata kusema nimekosa.”
Hicks amesema alikuwa amekasirishwa na ameghadhibishwa na kule kuwa aliamini familia ya watu watatu hawa walikuwa wanachukuwa eneo kubwa la kuegesha magari katika jengo hilo.
Waendesha mashtaka wanasema familia hiyo iliyouawa haikuwa inaegesha magari katika eneo la Hicks, na wameeleza kuwa aliwauwa kwa sababu walikuwa Waislam.
Familia ya wahanga hao ilitaka kufuatilia kufungua mashtaka ya jinai ya chuki yaliyoko katika sheria ya serikali kuu dhidi ya Hicks, lakini wapelelezi wanasema hakuna ushahidi wa kutosha juu ya madai hayo ya chuki.