Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 19:15

Maziko ya Nkaissery yatangazwa rasmi Kenya


Marehemu Joseph Nkaissery
Marehemu Joseph Nkaissery

Aliyekuwa Waziri wa Usalama Kenya Joseph Nkaissery atazikwa Jumamosi katika eneo lake huko Ilbisil kaunti ya Kajiado.

Kamati ya maziko, inayoongozwa na Waziri wa Afya Cleopa Mailu, Jumatatu ametangaza kuwa ibada maalum itafanyika katika kanisa la Baptist Church Nairobi lilioko barabara ya Ngong Alhamisi, gazeti la Daily Nation limeripoti.

“Ibada hiyo itaanza saa 9:30am na itakuwa kwa watu wote,” tamko hilo limesema.

Kamati hiyo imeongeza kuwa madaftari ya maombolezo yatawekwa kuanzia Jumatano kwenye Jumba la Harambee, KICC, Kanisa la Baptist Church na makao makuu ya kauti zote 47.

Kamati hiyo inahusisha familia ya Nkaissery na maafisa wa serikali.

Meja-Jenerali mstaafu Nkaissery aliaga dunia Jumamosi usiku. Sababu za kifo chake bado hazijajulikana wakati wachunguzi wanakusanya taarifa kuhusu mida yake ya mwisho ilikubaini kilichomtokea kupelekea kifo chake.

XS
SM
MD
LG