Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 13:58

Nkaissery alipata maumivu ya kifua, na kupoteza fahamu


Marehemu Joseph Nkaissery

Waziri wa Usalama Kenya Joseph Nkaissery alikuwa amelalamika ana maumivu makali ya kifuani muda mfupi kabla ya kupoteza fahamu.

Baadaye ikatangazwa kwamba ameaga dunia mapema Jumamosi asubuhi, vyanzo vya habari katika familia vimeliambia gazeti la the Nation.

Habari hizi zimepatikana wakati Rais Uhuru Kenyatta Jumamosi akifanya mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Taifa ikulu, Nairobi na kumchagua Waziri wa Elimu Fred Matiang’i kukaimu nafasi ya mambo ya ndani.

Wakati maafisa upelelezi wanaendelea kupekuwa sehemu mbalimbali ambapo waziri huyo aliyefariki alikuwepo mida alipofikwa na umauti- likiwemo eneo la Bomas la Kenya na makazi yake huko Karen- maelezo yameendelea kupatikana kuhusu dakika zake za mwisho kabla ya kuaga dunia.

Polisi inasemekana wamechukua sampuli mbalimbali kutoka nyumbani kwake na katika Hoteli ya Bomas.

Meja Generali mstaafu Nkaissery imeripotiwa aliwasili katika makazi yake huko Karen mnamo saa 9pm na alikula chakula cha usiku na familia yake.

Inasemekana alikuwa amepita Hoteli ya Bomas kabla ya kuelekea nyumbani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG