Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 09:08

Nigeria yafanya shambulizi kubwa la anga dhidi ya majambazi


Wasichana waliokuwa wametekwa nyara kutoka shule ya bweni huko Zamfara, Nigeria, baada ya kuachiliwa Machi 2, 2021. Picha na REUTERS/Afolabi Sotund
Wasichana waliokuwa wametekwa nyara kutoka shule ya bweni huko Zamfara, Nigeria, baada ya kuachiliwa Machi 2, 2021. Picha na REUTERS/Afolabi Sotund

Ndege za kijeshi za Nigeria zimefanya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la wanamgambo majambazi, na kuwauwa takriban watu 100 wenye silaha huko Kaskazini Magharibi mwa nchi, vyanzo viwili vya jeshi vinavyofahamu operesheni hiyo pamoja na wakaazi wa eneo hilo walisema.

Jeshi la anga la Nigeria limethibitisha kuwa limefanya mashambulizi ya mabomu katika jimbo la Kaskazini Magharibi la Zamfara siku ya Jumanne, lakini msemaji alisema bado hawezi kutoa maelezo kuhusu idadi ya waliouawa.

Majimbo ya Kaskazini-Magharibi na katikati mwa Nigeria kwa miaka mingi yamekuwa yakitishwa na magenge, yanayojulikana katika meneo hayo kama majambazi, ambao huvamia vijiji, kuua na kuwateka nyara wanavijiji kwa ajili ya kudai fidia katika maeneo hayo ambavyo uwepo wa serikali ni dhaifu.

Magenge hayo, maarufu kwa utekaji nyara mkubwa kwenye shule na vyuo katika miaka ya hivi karibuni, yamejificha katika kambi kwenye msitu mkubwa unaozunguka majimbo ya Zamfara, Katsina, Kaduna na Niger.

"Ndege za kivita zilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya majambazi, nina uhakika zaidi ya 100 waliuawa na takriban mara mbili ya idadi hiyo wamejeruhiwa vibaya," mmoja wa maafisa wa kijeshi waliohusika katika operesheni hiyo alisema.

Afisa mwingine wa jeshi pia alithibitisha idadi hiyo. Wote wawili walizungumza na shirika la habari la AFP bila kutaja majina yao kwa sababu hawakuwa na mamlaka ya kuzungumza kuhusiana na operesheni hiyo.

Wakaazi wawili wa eneo hilo ambao waliielezea miili hiyo baada ya mashambulizi, pia walitoa idadi sawa.

Alipoulizwa kutoa maelezo zaidi, msemaji wa jeshi la anga la Nigeria Commodore Edward Gabkwet alithibitisha mashambulizi hayo ya anga.

"Lakini siwezi kukuthibitishia idadi ," alisema.

Shambulio hilo la anga lilikuwa ni operesheni ya pili kubwa ya anga dhidi ya majambazi huko Zamfara tangu 2015 wakati jeshi lilipopelekwa kupambana na magenge hayo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG