Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 00:39

Rais wa Nigeria apendekeza nyongeza ya kima cha chini cha mshahara


Rais wa Nigeria Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Tinubu

Rais wa Nigeria Bola Tinubu Jumapili alipendekeza nyongeza ya kima cha chini cha mshahara na bei nafuu ya usafiri wa umma unaotumia petroli miongoni mwa hatua nyingine za kusaidia kukabiliana na athari za mageuzi yake ya kiuchumi, huku vyama vya wafanyakazi vikitishia kuitiisha mgomo wa kitaifa.

Akizungumza kwenye televisheni ya taifa kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa nchi yake, tangazo la Tinubu limekuja baada ya kuondoa ruzuku ya muda mrefu ya mafuta ambayo iliigharimu serikali mabilioni ya dola kwa mwaka na kuifanya biashara huria ya sarafu ya naira.

Maafisa wa serikali wanasema mageuzi hayo yalikuwa yanahitajika ili kufufua uchumi wa taifa hilo na wawekezaji walipongeza mageuzi hayo, lakini Wanigeria wanasumbuka na kupanda mara tatu kwa bei ya mafuta na mfumuko wa bei ambao umefikia sasa asilimia 25.

Forum

XS
SM
MD
LG