Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:03

Nigeria: Serikali ya Jimbo yachunguza shambulizi la anga lililowaua wafugaji 27


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Polisi nchini Nigeria wamethibitisha ripoti  kwamba shambulizi jingine  la  anga  la jeshi lililokuwa linawalenga waasi, limewaua wafugaji 27 katika  jimbo la Nasarawa  lililopo kaskazini katikati mwa Nigeria. Shambulio kama hili liliuwa raia 64 Desemba 2022.

Polisi nchini Nigeria wamethibitisha ripoti kwamba shambulizi jingine la anga la jeshi lililokuwa linawalenga waasi, limewaua wafugaji 27 katika jimbo la Nasarawa lililopo kaskazini katikati mwa Nigeria. Shambulio kama hili liliuwa raia 64 Desemba 2022.

Tukio la karibuni limetokea katika jamii ya Rukubi huko Doma, eneo la serikali ya mtaa ya jimbo la Nasarawa usiku wa Januari 24, 2023. Msemaji wa Kituo cha Polisi cha Jimbo la Nasarawa Ramhan Nansel amethibitisha tukio hilo.

Kulingana na vyanzo vya habari, shambulizi hilo liliwalenga watu walioshukiwa ni majambazi ambao wamekuwa wakiwatisha wakazi wanaoishi katika maeneo ya mpakani yanayo unganisha majimbo ya Nasarawa na Benue.

Ansel alisema Kituo cha Polisi kinashirikiana na vyombo vingine vya usalama, na serikali ya jimbo kujua mazingira ambayo yalipelekea shambulio hilo la bomu, na kuwakamata wahusika.

“ Inasikitisha jambo kama hili limetokea. Wafugaji 27 wameuawa baada ya bomu kulipuka katika halmashauri ya Doma. Polisi na vyombo vingine vya usalama vinafanya kazi usiku kucha kutaka kufahamu kitu kilichosababisha shambulio hilo na kuwasaka waliohusika na kitendo hicho.

"Ni bahati mbaya kwamba jambo kama hilo lilitokea. Wafugaji 27 waliuawa baada ya bomu kulipuka katika Halmashauri ya Doma. Polisi na vyombo vingine vya usalama vinafanya kazi usiku kucha kufahamu kilichosababisha shambulio hilo na kuwasaka waliohusika na kitendo hicho,” alisema. (naona umeandika twice)

Akijibu kuhusu tukio hilo, Gavana wa Jimbo la Nasarawa Abdullahi Sule ameapa kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na mauaji ya wafugaji wanakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG