Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 15:14

Nigeria: Abiria waliokuwa wanasubiri treni wametekwa nyara na watu wenye silaha


Maktaba: mama akionyesha picha ya mtoto wake waliyetekwa nyara katika tukio lingine la watu wenye silaha kuteka watu nyara nchini Nigeria
Maktaba: mama akionyesha picha ya mtoto wake waliyetekwa nyara katika tukio lingine la watu wenye silaha kuteka watu nyara nchini Nigeria

Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wamewateka nyara abiria kadhaa waliokuwa wanasafiri kwa gari moshi kusini mwa Nigeria.

Polisi wamesema kwamba watu hao walikishambulia kituo cha gari moshi katika mji wa Igueben, jimbo la Edo na kutwaeka nyara watu kadhaa waliokuwa wanasubiri kusafiri.

Msemaji wa polisi katika jimbo la Edo Chidi Nwabuzor, amesema kwamba watu hao walifyatua risasi kadhaa hewani kabla ya kuwateka abiria.

Baadhi ya abiria walijeruhiwa, na polisi wamesema kwamba juhudi za uokoaji zinaendelea.

Watu saba waliuwawa na wengine kadhaa kutekwa nyara mwaka uliopita katika shambulizi dhidi ya kituo cha treni karibu na mji mkuu wa Abuja.

XS
SM
MD
LG