Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:18

Mlipuko wa bomu waua wafugaji 27 nchini Nigeria, polisi wasema


Ramani ya Nigeria
Ramani ya Nigeria

Wafugaji 27 waliuawa Jumatano na wengine kadhaa kujeruhiwa katika kile polisi wamekiita mlipuko wa bomu katikati mwa Nigeria, eneo lenye mivutano ya kikabila na kidini.

Wafugaji hao na ng’ombe wao walikuwa katika kijiji cha Rukubi kinachopatikana kwenye mpaka kati ya majimbo ya Nasarawa na Benue wakati bomu lilipolipuka katikati yao.

“Tumegundua watu 27 waliuawa katika mlipuko wa bomu pamoja na ng’ombe kadhaa, alisema Maiyaki Muhammed Baba, kamishna wa polisi wa Nasarawa.

Amesema “ Watu wengine wengi walijeruhiwa na idadi ya vifo inaweza kuongezeka”, akiongeza kuwa wataalam wa mabomu wamekuwa wakichunguza chanzo cha mlipuko huo.

Lakini chama kinachowakilisha wafugaji kimesema mlipuko huo ulisababishwa na shambulizi la anga la kijeshi.

“Lilikuwa shambulizi la anga. Liliuawa watu wetu 27,” amesema Lawal Dano wa shirika la wafugaji wa ng’ombe, Miyetti Allah Cattle Breeders.

XS
SM
MD
LG