Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 06:30

Nchi wanachama wa NATO zatia saini itifaki kwa ajili ya azma ya Sweden, Finland kujiunga


Viongozi wa Sweden and Finland wakikutana na Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg (Katikati) mjini Brussels, Ubelgiji

Nchi wanachama wa NATO, leo zimetia saini nyaraka za itifaki, hiyo ikiwa ni hatua nyingine muhimu, katika mchakato wa azma ya Finland na Sweden kujiunga muungano huo wa kijeshi.

Nchi zote mbili ziliwasilisha maombi ya kujiunga na NATO mwezi Mei mwaka huu, kinyume na misimamo ya muda mrefu, ya kutofungamana na upande wowote katika kukabiliana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

"Hii ni siku nzuri kwa Finland na Sweden, na siku nzuri kwa NATO,” amesema Katibu Mkuu wa NATO, Jen Stoltenberg.

“Kwa kuwa mataifa 32 yametia saini itifaki hizi, tutakuwa na nguvu zaidi na watu wetu watakuwa salama zaidi tunapokabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa usalama katika miongo kadhaa," Stoltenberg aliongeza.

Aliendelea kusema kuwa mlango wa NATO bado uko wazi kwa “demokrasia za Ulaya ambazo ziko tayari kuchangia usalama wetu wa pamoja."

Baada ya itifaki za kujiunga kutiwa saini, kila moja ya nchi wanachama wa NATO, sasa zinapaswa kuziidhinisha azma hiyo ya Finland na Sweden, kulingana na taratibu zao za kitaifa.

Licha ya makubalino katika umoja huo, pingamizi la awali ya mjumbe Uturuki linaweza kusababisha matatizo kwa ajili ya kukamilisha uanachama.

Wiki iliyopita rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdowan alionya kwamba Ankara inaweza kuendelea kuzuia utaratibu huo, kama nchi hizo mbili zitashindwa kufikia matakwa ya uturuki kuwarejesha washukiwa wa ugaidi wenye uhusiano na makundi haramu ya kikurdi au mtandao wa kiongozi wa kidini aliyoko uhamishoni anayeshutumiwa kwa mapinduzi yaliyoshindwa ya mwaka 2016 huko uturuki.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG