Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:57

Waziri mkuu wa Australia kuhudhuria kikao cha NATO


Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese
Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese

Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese Jumatatu anasafiri kuelekea Uhispania ili kuhudhuria mkutano wa NATO wa mwaka huu, wakati viongozi wakitadhmini kuhusu ukosefu wa usalama kote ulimwenguni.

Albanese ataungana na wenzake kutoka New Zealand, Japan na Korea kusini, nchi ambazo si wanachama wa ushirika huo na hivyo kufanyika kikao kikubwa zaidi cha kawaida cha NATO.

Ingawa mataifa hayo manne siyo wanachama wa NATO, mchango wao ni muhimu kwa kuwa unaleta mchango wa kanda ya Indo Pacific kwenye usalama wa ulimwengu. Uvamizi wa Russia nchini Ukraine unatarajiwa kupewa kipaumbele wakati wa mkutano huo unaofanyikia mjini Madrid.

Wachambuzi wanaamini kwamba NATO itakemea China kutokana na msimamo wake wa kutolaumu Russia kutokana na uvamizi huo. Albanese anazuru Ulaya kwa mara ya kwanza ikiwa waziri mkuu wa Australia tangu kuchukua madaraka mwezi Mei.

XS
SM
MD
LG