Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:01

Marekani kuongeza zaidi uwepo wake wa kijeshi Ulaya


Rais wa Marekani, Joe Biden
Rais wa Marekani, Joe Biden

Rais wa Marekani, Joe Biden, Jumatano ametangaza Marekani inaongeza uwepo wake wa kijeshi barani Ulaya.

Hatua hiyo inajumuisha pamoja na kuongeza vifaa zaidi vya jeshi la baharini Uhispania, na kuongeza vikosi vyake katika maeneo mengine zaidi.

Akihutubia mkutano wa mataifa 30 ya NATO, rais Biden amesema Marekani itaanzisha kambi kuu ya kudumu ya 5 ya Marekani nchini Poland, kuongeza kikosi cha wanajeshi 5,000, na wengine 2,000 watakaowekwa katika kambi ya Romania, na kutuma ndege zaidi mbili za F-35 kwenda Uingereza.

Akiwa jijini Madrid, rais Biden, amesema anatangaza kuongeza nguvu ya Marekani barani Ulaya kutokana na mazingira yaliyo badilika ya kiusalama, pamoja na kuboresha juhudi za pamoja za usalama.

Viongozi wa NATO wanajadili kuongeza msaada kwa Ukraine na namna muungano wao wa toka vita vya pili vya dunia utakabiliana na changamoto za sasa na zijazo.

XS
SM
MD
LG