Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 14:31

Nahodha atelekeza meli ikiwa na wahamiaji 400 baharini


Manusura wa mashua ya wahamiaji iliyopinduka wakiwa jirani na kisiwa cha New Providence, Bahamas, Julai 24, 2022. Picha na Kitini / Jeshi la Ulinzi la Royal Bahamas / AFP.
Manusura wa mashua ya wahamiaji iliyopinduka wakiwa jirani na kisiwa cha New Providence, Bahamas, Julai 24, 2022. Picha na Kitini / Jeshi la Ulinzi la Royal Bahamas / AFP.

Meli iliyokuwa imebeba takriban watu 400 imepoteza mwelekeo na kuanza kujaa maji ikiwa katika meneo ya kati ya Ugiriki na kisiwa cha Malta.

Huduma ya msaada ya Alarm Phone ilisema siku ya Jumapili, kufuatia ongezeko kubwa la boti zikiwa zimebeba wahamiaji zikivuka bahari ya Mediterania zikitokea Afrika Kaskazini.

Shirika lisilo la kiserikali la Ujerumani Sea-Watch International lilisema kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa limeipata boti hiyo ikiwa na meli mbili za wafanyabiashara karibu yake. Lilisema shirika hilo kuwa mamlaka ya Malta iliziamuru meli hizo kutofanya uokoaji na kwamba moja kati ya meli hizo iliombwa kuijaza mafuta.

Haikuwezekana kwa haraka kuifikia mamlaka ya Malta kutoa maoni.

Alarm Phone ilisema kupitia mtandao wa Twitter kuwa ilipokea simu kutoka kwenye boti hiyo, iliyokuwa ikisafiri usiku kucha ikitokea katika jiji la Tobruk, nchini Libya, na kuziarifu mamlaka. Lakini mamlaka haijaanzisha operesheni ya uokoaji mpaka sasa, waliongeza.

Huduma hiyo ya simu ilisema boti hiyo kwa sasa iko katika eneo la Uokoaji na Utafutaji (SAR) katika kisiwa cha Malta. Alarm Phone imesema watu waliokuwemo kwenye meli hiyo walikuwa katika taharuki, ambapo wengi wao wakihitaji matibabu.

Tukio hilo lilitokea baada ya Meli hiyo kuishiwa mafuta na sitaha yake ya chini kujaa maji, wakati nahodha alipoitelekeza boti hiyo ambayo ilikosa mtu wa kuiendesha walisema.

Chanzo cha habari hii nis Shirika la Habari ka Reuters.

XS
SM
MD
LG