Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:34

Watu 40 wafariki katika kituo cha wahamiaji nchini Mexico


Watu waandamana nje ya kituo cha wahamiaji cha Mexico baada ya moto kuzuka katika kituo hicho, Machi 28, 2023
Watu waandamana nje ya kituo cha wahamiaji cha Mexico baada ya moto kuzuka katika kituo hicho, Machi 28, 2023

Takriban watu 40 wamefariki na wengine 29 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka Jumanne kabla ya Alfajiri katika kituo cha wahamiaji cha Mexico kwenye mpaka na Marekani.

Kituo hicho katika mji wa Mexico wa Ciudad Juarez kilikuwa kinawahifadhi wanaume 68 kutoka Amerika ya kati na Amerika kusini, ambalo ni eneo kuu la kuvuka mpaka kwa wahamiaji au waomba hifadhi wanaotaka kuingia Marekani.

Waliofariki na kujeruhiwa ni kutoka Guatemala, Honduras, El Salvador, Venezuela, Colombia na Ecuador.

Waziri wa mambo ya nje wa Guatemala Mario Bucaro alisema 28 kati ya waliokufa ni raia wa Guatemala.

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador alisema wahamiaji waliposikia kuwa watarudishwa katika nchi zao kutoka Mexico, walianza kuchoma moto ndani ya kituo hicho kupinga kurudisha makwao.

XS
SM
MD
LG