Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:42

Mwandishi wa Tanzania aahidi kuendelea kupigania uhuru wa habari


Mtandao wa jamiiforums ukiwa na wasifu na picha ya muanzilishi mwenza Maxence Melo Mubyazi
Mtandao wa jamiiforums ukiwa na wasifu na picha ya muanzilishi mwenza Maxence Melo Mubyazi

Maxence Melo anasema “hakupanga kuwa mwandishi wa habari.” Anasema tovuti aliyoianzisha nchini Tanzania, Jamii Forums, inalengo la kawaida : kuwapa vijana sauti, kuwapa nafasi kuwa huru kujieleza na kupambana na ufisadi.

Lakini athari ya tovuti hiyo na hatua inayochukua serikali ya Tanzania zimekuwa ni kiurahisi. Melo amefikishwa mahakamani mara 137 katika kipindi cha miaka mitatu, amekamatwa mara mbili na kukaa jela kwa siku 14.

“Nilikabiliwa na vipingamizi vingi kuhusiana na uhuru wangu lakini najua ni thamani tunayolipa kwa sababu ya msingi wa uhuru wa namna hii,” ameiambia VOA.

Wiki hii Melo ametunukiwa tuzo ya Uhuru wa Vyombo vya Habari vya Kimataifa iliyotolewa na Kamati ya Kimataifa ya Kuwalinda Waandishi, CPJ. Ameungana na waandishi kutoka Brazil, India na Nicaragua katika kupokea tuzo yenye heshma ya kipekee.

Jamii Forums

Jamii Forums ilianzishwa mwaka 2006, na huchapisha habari zake kwa lugha ya Kiswahili na inawasomaji Tanzania, Kenya na Uganda. Ilipata sifa mbaya mwaka 2007 kufuatia habari inayohusu ufisadi uliokuwa umetokea Benki Kuu ya Tanzania, ambapo milioni ya dola za Marekani zilikuwa zimechukuliwa. Melo alisema kuwa mwanzoni tovuti hiyo ilikuwa inapokea vitisho rasmi na mamlaka nchini Tanzania walikuwa wanataka kujua nani anaendesha safu hiyo.

Mwaka 2008 tovuti hiyo ilichapisha habari ikianika ufisadi katika mikataba ya mashine za kufua umeme ambayo hatimaye ilipelekea waziri mkuu kujiuzulu na baraza la mawaziri kuvunjwa. Melo alisema anaendelea kufuatiliwa kuanzia wakati ule.

Anasema maafisa wa serikali, wabunge na wanachama wa vyama vya upinzani aghlabu wanaingia katika safu ya Jamii Forums na kujadiliana na watumiaji wengine wa safu hiyo. Anasema kuwa ghadhabu anazokabiliwa nazo kutoka kwa mamlaka siyo juu ya kuchapisha habari potofu, ni juu ya kuripoti habari ambazo maafisa hao wa serikali hawazipendi.

Mazingira ya vyombo vya habari yalifikia kuwa hatarishi zaidi mwaka 2015 wakati Tanzania ilipopitisha Sheria ya Uhalifu wa Mitandao. Sheria hiyo inafanya ni kosa la jinai mazungumzo yote ya mitandaoni inayofikiria kuwa ni uongo, udanganyifu, inapotosha au siyo sahihi. Sheria hiyo imetumika kuwafungulia mashtaka mitandao ya habari kama vile Jamii Forums.

“Sheria hiyo haitumiki tu dhidi ya waandishi wa habari au dhidi ya waandishi wasiokuwa katika tasnia, inatumika dhidi ya sauti yoyote inayokosoa. Takriban inatumika dhidi ya kila mtu,” amesema .

Sheria nyingine za ziada inawazuia waandishi kupata habari za serikali na takwimu, ameeleza Mela.

Lakini Melo amesema bado anayo azma ya kuendelea kujishughulisha na uandishi nchini Tanzania.

“Tanzania imekuwa ni mfano mzuri Afrika,” amesema. “Sisi tumekuwa ni mabalozi wa mabadiliko Afrika. Na tumepitia katika nyakati zenye changamoto kama hizi kwa takriban miaka mitano zinazowakabili waandishi – na sauti za wakosoaji nchini Tanzania. Mimi bado nina matumaini kuwa ipo fursa ya kuleta mabadiliko. Na sisi kama raia tunafursa ya kuomba mabadiliko katika sera.”

Amekwenda mahakamani kupinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Uhalifu wa Mitandao bila ya mafanikio lakini hajakata tamaa.

XS
SM
MD
LG