Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:19

Jamii Forums yasitisha huduma; mazungumzo na TCRA yaendelea


TCRA
TCRA

Mtandao wa Jamii Forums nchini Tanzania umechukua hatua ya kusitisha huduma zake kutokana na hatua ya mamlaka ya mawasiliano nchini humo kutaka mitandao kusajiliwa na kupewa leseni kufikia Juni 11, 2018.

Akizungumza na idhaa ya Kiswahili VOA Jumatatu mwanzilishi mwenza wa mtandao wa Jamii Forums, Mike Mushi aliyeko Arusha, Tanzania, amesema kanuni hiyo mpya ina vipengere ambavyo ni shida kuvitimiza.

“Ikiwa tutakubali kufanya hivyo ina maana tutakuwa tunaingilia faragha ya watumiaji wetu. Kanuni pia inalazimisha kufanya kazi na vyombo vya ulinzi na usalama. Lakini kanuni inalazimisha kuwa taarifa za watu lazima tuzitume kwa kipindi cha miezi 12,” ameeleza.

Kifungu cha 5,e, cha kanuni ya sheria mpya ya mtandaoni kinasema ni lazima uweke njia za kupata taarifa binafsi za wachangiaji wanaoweka maudhui kwenye mtandao husika.

Kwa upande wa mitandao ya kimataifa Kanuni imewaondolea kizuizi, wao hawaguswi na kanuni hii, lakini Watanzania wote ni lazima wachukue leseni.

Bado tunatafuta njia ya kukaa na TCRA na kuwaelewesha, kwa kuongea nao na kufikisha ujumbe wetu na kuelezea kitu hiki kitakuwa kigumu kwa upande wetu.

“Ni matumaini yetu mazungumzo haya yatazalisha matunda chanya ili jamii forums iweze kurudi hewani.

XS
SM
MD
LG