Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 11:59

Mwanaharakati wa Ghana akamatwa kwa "kutishia kuipindua serikali"


Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo

Mwanaharakati maarufu wa wa kutetea haki za raia nchini Ghana ambaye amekuwa akiongoza maandamano dhidi ya serikali ya Rais Nana Akufo-Addo, alikamatwa Jumamosi baada ya kutoa maoni kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu "kupanga njama ya mapinduzi."

Posisi wa Ghana wamesema kwamba Oliver Barker-Vormawor, kiongozi wa kundi liitwalo #FixTheCountry, ambalo limekuwa likiongoza maandamano katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuishutumu serikali kwa ajili ya matatizo ya kiuchumi miongoni mwa masuala mengine, alikamatwa na kuzuiliwa katika uwanja wa ndege siku ya Ijumaa, alipowasili kutoka Uingereza.

Barker-Vormawor aliandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba atafanya mapinduzi iwapo Bunge litapitisha mswada tata, uitwao E-Levy.

Mswada huo unapendekeza kodi ya asili mia 1.75 kwa miamala ya kielektroniki ikijumuisha malipo ya pesa kwa njia ya simu.

"Ikiwa E-Levy itapita ... nitafanya mapinduzi mwenyewe. Jeshi lisilo na maana!" Barker-Vormawor alisema katika ukurasa wake wa Facebook.

"Maandishi hayo yalikuwa na taarifa ya wazi ya nia ya kutekeleza mapinduzi.. nia ya kupindua katiba ya Jamhuri ya Ghana," polisi walisema katika taarifa.

Mshukiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG