Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:59

Ghana kupiga faini wasafiri wa ndege wasiopigwa chanjo ya Covid


Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo akiongza kikao mapema mwaka huu.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo akiongza kikao mapema mwaka huu.

Idara ya safari za ndege inayomilikiwa na serikali ya  Ghana imesema Jumatatu kwamba mashirika ya ndege yataanza kutoza faini ya dola 3,500 kwa kila msafiri anayewasili nchini humo bila kupokea chanjo kamili ya Covid19.

Hatua hiyo inaonekana kuwa hatua ya karibuni zaidi kwenye taifa hilo lenye kanuni kali zaidi kieneo. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, mashirika ya ndege pia yatatozwa faini sawa na hiyo kwa kila msafiri ambaye hakujaza fomu kuhusiana na afya yake kabla ya kuingia ndege kuelekea kwenye uwanja wa kimataifa wa Kokota mjiji Accra.

Hata hivyo raia wa Ghana waliosafiri kwenye mataifa ya nje wataruhusiwa kuingia tena nchini mradi wajiweke kwenye karantini ya lazma ya siku 14 iwapo hawajapokea chanjo, huku wageni wakiwa na uwezekano wa kutoruhusiwa kuingia nchini humo.

Ghana yenye takriban wakazi milioni 31 ni moja wapo ya mataifa yenye mfumo bora zaidi wa upimaji wa corona Afrika magharibi wakati ikiwa na kesi 132,000 za maambukizi na vifo 1,243 tangu janga la corona lilipoingia mwaka jana.

XS
SM
MD
LG