Bunge hilo limegawanyika kati ya vyama vikuu viwili kufuatia uchaguzi wa mwaka mmoja uliopita, suala ambalo huenda likahujumu juhudi za taifa hilo za kujikwamua kiuchumi kutokana na athari za janga la corona.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP,wakati wa kura ya Ijumaa iliyopita, wabunge wa chama tawala cha New Patriotic NPP waliondoka bungeni kutokana na madai kwamba spika ambaye ni wa upinzani alipendelea upande mmoja kwa kusema kwamba waziri wa fedha asiwepo bungeni wakati wa shughuli hiyo.
Basi hapo ndipo upinzani ulipata nafasi ya kupiga kura ya kupinga pendekezo hilo ikiwa mara ya kwanza kufanyika tangu mwaka 1981.Licha ya wabunge wa upinzani kususia kura ya Jumanne, spika mwandamizi Osei Owusu kutoka chama tawala cha NPP alitangaza kupitishwa kwa bajeti hiyo akisema kwamba imepata wingi wa kura.