Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:50

Mwanafunzi wa sekondari auawa kinyama Uganda


washukiwa wakamatwa Uganda
washukiwa wakamatwa Uganda

Polisi wanawashikilia wanafamilia wawili kwa shutma za kushiriki katika mauaji ya Norah Wanyana.

Marehemu Wanyana ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jeshi la Anga Entebbe, Uganda alikutwa amekufa na wakazi wa eneo la Nkumba.

Wanaoshikiliwa ni Mohammed Ssebaduka na ndugu yake ambaye ana umri wa miaka 17. (Jina limehifadhiwa)

Mwili wa marehemu uliokuwa umevuliwa nguo zote uligunduliwa Ijumaa iliopita na kipande cha kijiti kimekutwa kimewekwa kwenye sehemu zake za siri.

Mkuu wa Kituo kikuu cha polisi cha Entebbe Zachariah Mbabazi amethibitisha kukamatwa watu hao wawili ambao ni ndugu.

“Ndio wamewekwa rumande na inapendelewa kuwa watafunguliwa mashtaka ya uuaji, na tutawapeleka mahakamani muda sio mrefu,” amesema.

XS
SM
MD
LG