Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 17:00

Museveni aelekea kupata ushindi mkubwa


Wananchi wakipiga kura Nakasero Ijumaa

Mpinzani mkuu Kizza Besigye asema kulikuwa na wizi mkubwa wa kura katika uchaguzi wa mwaka huu, zaidi ya uchaguzi wa 2006

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anaelekea kupata ushindi mkubwa katika uchuguzi mkuu wa nchi hiyo. Huku hesabu ya kura ikiendelea kutolewa hadi kufikia Jumamosi jioni Rais Museveni alikuwa anaongoza kwa zaidi ya asilimia 70 ya kura zote.

Mpinzani wake mkuu Dr. Kizza Besigye wa IPC, muungano wa vyama kadha, alikuwa na asilimia 23 hadi majira ya jioni. Lakini Dr. Besigye alisema jumamosi jioni kuwa kulikuwa na wizi mkubwa wa kura katika uchaguzi wa mwaka huu, zaidi ya vile ilivyokuwa mwaka 2006 kama anavyodai.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi jioni Dr. Besigye alisema atakutana na wanachama wa IPC Jumapili kujadili hatua ifuatayo.

Machafuko ya hapa na pale yameripotiwa katika baadhi ya vituo vya kuhesabia kura kutokana na kucheleweshwa kwa kutangazwa kwa matokeo katika vituo hivyo.

XS
SM
MD
LG