Uchaguzi mkuu wa Uganda umegubikwa na ghasia na malalamiko ya kasoro za uchaguzi wakati wapiga kura walipokua wanapiga kura katika uchaguzi mkuu siku ya Ijuma Februari 18, 2011.
Katika sehemu nyingi za nchi inaripotiwa kwamba uchaguzi umefanyika kwa amani lakini katika vituo vingi wapiga kura wamelalamika kwamba hawakuona majina yao kwenye daftari ya majina ya wapigaji kura.
KUna baadhi ya wapiga kura pia wanalalamika kwamba walipofika kwenye vituo wameambiwa kwamba kuna alama kando ya majina yao ikimaanisha wamepiga kura.
Mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni katika kugombania kiti cha rais Dk. Kiza Besigye, alilazimika kwenda kupiga kura katika kituo kipya baada ya kuambiwa kwamba jina lake halikuandikwa kwenye kituo ambacho kawaida yeye hupigia kura.