Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:17

Museveni ashinda uchaguzi Uganda


Wafanyakazi wakihesabu kura baada ya uchaguzi Uganda
Wafanyakazi wakihesabu kura baada ya uchaguzi Uganda

Awamu nyingine ya miaka mitano itamwezesha Rais Museveni kukaa madarakani Uganda kwa kipindi cha miaka 30

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa kwa kupata asilimia 68.38 ya kura 8,272,760 zilizopigwa katika uchaguzi huo. Bw. Museveni alipata jumla ya kura 5,428,369, kulingana na tamko la mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Badru Kiggundu.

Mpinzani wa miaka mingi Dr. Kizza Besigye ambaye aligombania kwa tiketi ya muungano wa chama cha IPC alipata asilimia 26 ya kura. Hata hivyo, saa kadha kabla hata matokeo rasmi kutangazwa chama cha IPC kilitamka kuwa kinapinga matokeo ya uchaguzi huo.

Katika taarifa yake IPC ilitoa sababu kadha ya kupinga matokeo ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha kurubuni utaratibu mzima, madai ya kwamba kumepatikana masanduku kadha ya kura ambazo zilipigwa kabla na kujazwa katika masanduku hayo.

Hata hivyo, Dr. Besigye hajatoa tamko rasmi tangu matokeo rasmi kutangazwa.

XS
SM
MD
LG