Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 09:29

Mtoto wa miaka 13 apambana na simba Tanzania


Tanzania

Simba ambaye alimshambulia mtoto wa miaka 13 wa kiume na kumjeruhi vibaya katika eneo la paja lake la kulia nchini Tanzania hakufanikiwa katika windo lake.

Mtoto huyo Nyutuliangila Madirisha inaelezwa juu ya ushujaa wake baada ya kuamka kutoka usingizini alimshambulia mnyama huyo aliyekuwa akimpapasa kwa kumpiga ngumi ya uso.

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vinasema kuwa kutokana na tukio hilo, mtoto huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Isinde mkoani Katavi, amelazwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa matibabu kutokana na majeraha ya paja lake la kulia baada ya simba huyo kumshambulia.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mpanda, Dk Theopister Elisa amethibitisha kuwa mtoto huyo amepokelewa na kulazwa hospitalini hapo kwa matibabu, akiwa amejeruhiwa paja lake la mguu wa kulia.

Akiwa hospitali amesimulia tukio hilo akisema alikuwa amelala fofofo pembeni mwa zizi la ng’ombe lililopo nyumbani kwao, lakini alishituka ghafla usingizini baada ya kuhisi kuwa alikuwa akipapaswa mwilini na mnyama.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Madirisha Lubinza ambaye pia anafuga mbwa wengi kwa ajili ya ulinzi, alieleza kuwa usiku wa tukio hilo alisikia kelele za mtoto wake akiomba msaada huku simba akiunguruma kwa nguvu.

Alidai baada ya kusikia sauti ya mwanawe akiomba msaada ndipo alipotoka na kuwaamuru mbwa wake, wamshambulie simba huyo ndipo walipoanza kumbwekea na kumtisha na baadaye simba huyo aliingiwa hofu na kukimbilia porini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG