Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 26, 2023 Local time: 04:48

Mwanamfalme Harry na mkewe Megan wahama kwenye kasri ya familia


Mwanamfalme Harry wa Uingereza, Duke wa Sussex na mkewe Meghan wakiwa London, tarehe 9 Machi 2020. Picha na Tolga AKMEN / AFP.

Maafisa wa Kasri ya Buckingham, ya mfalme wa Uingereza, wametangaza Alhamisi, kwamba Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan hatimaye wamehama nyumba waliokuwa wakiishi kwenye kasri ya familia ya kifalme ya Windsor, iliyoko magharibi mwa London, Palace ilithibitisha Alhamisi.

Nyumba hiyo, inayofahamika kama Frogmore Cottage, ilikuwa zawadi ya harusi waliyopewa wanandoa hao na bibi yake Harry, marehemu Malkia Elizabeth II, mwaka 2018.

Lakini ililiripotiwa walitakiwa kuondoa vitu vyao vyote vilivosalia siku chache baada ya Harry, mtoto wa mwisho wa Mfalme Charles III, kuanza kuikosoa vikali familia yake katika kitabu chake cha kumbukumbu chenye utata cha "Spare" mwezi Januari 2023.

"Tunaweza kuthibitisha kwamba Duke na Duchess wa Sussex wameondoka Frogmore Cottage," afisa mkuu wa kasri Michael Stevens alisema kama ripoti ya kila mwaka ya fedha ya kifalme ilichapishwa Alhamisi.

"Hatutaelezea kwa undani kuhusu mipango iliyopo," alisema Stevens, ambaye ni mweka hazina wa mfalme.

Aliongeza kusema kuwa wanandoa hao ambao kwa sasa wanaishi California wameshalipa pauni milioni 2.4 ambazo ni kodi na gharama za kukarabati kasri hiyo, ambayo ni mali ya mfalme.

Kunyan’ganywa nyumba hiyo kunawafanya wanandoa hao kutokuwa na makazi ya msingi nchini Uingereza.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG