Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 20:32

Uingereza yasema mpango wake wa kuzuia wahamiaji wanaoingia kwa boti umefanikiwa kwa asilimia 20


Rishi Sunak akiwa London.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak Jumatatu amesema mpango wake wa kuzuia wahamiaji wanaoingia kwa kutumia boti ndogo umepunguza watu kuvuka mpaka kwa asilimia 20, sahihisho ambalo anatumai litapunguza kukosolewa kutoka kwa chama chake na nchini juu ya sera yake ya uhamiaji.

Sunak, ambaye anatarajiwa kuongoza chama chake cha Conservative kwenye uchaguzi wa taifa mwaka ujao, aliahidi kuzuia boti kuvuka bahari ya Uingereza ikiwa moja ya ahadi zake tano baada ya kuingia madarakani mwezi Oktoba mwaka jana.

Lakini alikosolewa na wanachama wa chama chake na umma kwa kutosonga mbele haraka vya kutosha, huku watu wakiandamana kupinga kuwalaza mamia ya wahamiaji katika mahoteli baada ya idadi kubwa ya wahamiaji kuwasili Uingereza mwaka jana.

“Katika kipindi cha miezi mitano tangu nianzishe mpango huu, kuvuka mpaka kinyume cha sheria kumepungua kwa asilimia 20, ikilinganishwa na mwaka jana,” Sunak ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kusini mwa Uingereza.

Amesema mpango wake unafanya kazi, na kuongeza kuwa serikali yake haitachoka na itafanya kazi kwa bidi kuhakikisha bunge linapitisha sheria mpya kuhusu uhamiaji.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG