Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:11

Serikali ya Uingereza inataka kuwapeleka wahamiaji Rwanda zaidi ya kilomita 6,400


Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak (R) akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame huko Downing Street, London

Serikali ya ki-Conservative ya Waziri Mkuu Rishi Sunak inataka kuwapeleka maelfu ya wahamiaji zaidi ya kilomita 6,400 kwenda Rwanda kama sehemu ya makubaliano na nchi hiyo ya Afrika ya kati yaliyofikiwa mwaka jana

Mpango wa Uingereza wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda utagharimu paundi 169,000 sawa na dola 215,035 kwa kila mtu kulingana na tathmini ya kwanza ya serikali ya ahadi yenye umuhimu mkubwa ya kukabiliana na idadi kubwa ya watu wanaowasili nchini humo katika boti ndogo.

Serikali ya ki-Conservative ya Waziri Mkuu Rishi Sunak inataka kuwapeleka maelfu ya wahamiaji zaidi ya kilomita 6,400 kwenda Rwanda kama sehemu ya makubaliano na nchi hiyo ya Afrika ya kati yaliyofikiwa mwaka jana. Serikali inaona mpango huo kama muhimu kwa kuwazuia wanaotafuta hifadhi wanaowasili katika boti ndogo kutoka Ufaransa.

Sunak ameifanya hii kuwa moja ya vipaumbele vyake vitano huku kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wabunge wake wa Conservative na umma kutatua suala hilo, na chama chake kiko nyuma sana ya Chama kikuu cha upinzani cha Labour katika kura za maoni kabla ya uchaguzi wa kitaifa unaotarajiwa mwaka ujao.

Katika tathmini ya athari za kiuchumi iliyochapishwa Jumatatu, serikali ilisema gharama ya kumsafirisha kila mtu kwenda Rwanda, itajumuisha wastani wa malipo ya paundi 105,000 kwa Rwanda kwa ajili ya kumpokea kila mtafuta hifadhi, paundi 22,000 kwa safari ya ndege na msindikizaji, na paundi 18,000 kwa ajili ya utaratibu na gharama nyingine za kisheria.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Suella Braverman alisema gharama hizi lazima zizingatiwe pamoja na athari za kuzuia wengine kujaribu kufika Uingereza na ongezeko la gharama za wanaotafuta hifadhi ya makazi.

Forum

XS
SM
MD
LG