Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 07:53

Mtoto afariki na watu 23 hawajulikani walipo baada ya kiboko kugonga mtumbwi Malawi


Mtumbwi wa uokoajia ukiwa katika kijiji cha Chambuluka huko Nsanje, tarehe 18 Januari 2015. Picha na AFP/ AMOS GUMULIRA.
Mtumbwi wa uokoajia ukiwa katika kijiji cha Chambuluka huko Nsanje, tarehe 18 Januari 2015. Picha na AFP/ AMOS GUMULIRA.

Mtoto mchanga amefariki na watu wengine 23 hawajulikani walipo baada ya kiboko kugonga mtumbwi waliokuwa wakisafiria katika Mto Shire nchini Malawi, mamlaka ilisema siku ya Jumanne.

Polisi wa wilaya ya Nsanje, kusini mwa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika walisema chombo hicho cha majini, mtumbwi, ulikuwa umebeba watu 37 waliokuwa wakivuka mto huo wakati ajali ilipotokea Jumatatu asubuhi.

Msemaji wa polisi wa wilaya ya Nsanje, Agnes Zalakoma aliliambia shirika la AFP kuwa, wenyeji wa eneo hilo waliweza kuwatoa watu 13 kutoka kwenye maji hayo ya hatari, wakati mpaka Jumanne watu wengine 23 bado hawajajulikana walipo.

Waokoaji pia walipata maiti ya mtoto wa mwaka mmoja ambaye alikufa maji katika ajali hiyo, alisema.

Mtumbwi ulianza kusuasua na hatimaye kupinduka, baada ya kugongana na kiboko, Zalakoma alisema.

Shire ni mto mkubwa sana nchini Malawi.

Ajali za boti ni jambo la kawaida nchini Malawi, ambako ukosefu wa usafiri wa kawaida wa majini una walazimisha watu wengi kuvuka maziwa na mito kwa kutumia boti zilizochakaa na bila kufuata kanuni sahihi.

Mwezi uliopita watu takriban watano walifariki dunia, baada ya boti iliyokuwa imepakia watu kupita kiwango kuzama katika wilaya ya Mchinji iliyopo katikati mwa Malawi.

Chanzo cha bahari hii ni Shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG