Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 04:29
VOA Direct Packages

Maelfu waugua kipindupindu Msumbiji kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Freddy


Watu wakitembea kwenye maji ya mafuriko kwenye mji wa Quelimane, Msumbiji baada ya kimbunga Freddy.
Watu wakitembea kwenye maji ya mafuriko kwenye mji wa Quelimane, Msumbiji baada ya kimbunga Freddy.

Wiki kadhaa baada ya kimbunga Freddy kugonga Msumbiji kwa mara ya pili, taifa hilo ambalo bado limefurika, linashuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya kipindupindu kutokana na hali hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, kufikia Machi 27, zaidi ya visa 19,000 vya kipindupindu vilikuwa vimeripotiwa kote kwenye majimbo 8 ya Msumbiji, kulingana na ripoti kutoka afisi ya UN inayoratibu masuala ya kibinadamu, ikiwa ni ongezeko maradufu ndani ya wiki moja.

Kimbunga Freddy kinasemekana kuwa kirefu zaidi kikichukua zaidi ya wiki 5 na kugonga Msumbiji mara 2. Kiliuwa watu 165, Msumbiji, 17 Madagascar na 676 nchini Malawi. Zaidi ya watu 530 kufikia sasa hawajulikani walipo nchini Malawi wiki mbili baadaye, na hivyo huenda idadi ya vifo nchini humo ikavuka 1,200.

Watu 31 wameripotiwa kufa kutokana na kipindupindu kwenye hospitali ya mji mkuu wa jimbo la Zambezia wa Quelimane , huku wengine 3,200 wakilazwa hospitali kati ya Machi 15 na 29 kulingana na takwimu za wizara ya afya.

XS
SM
MD
LG