Tuzo hizo zitatolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo.
Tamko lilitolewa na Ikulu ya Marekani kupitia tovuti yake tuzo hizo zinatolewa kwa ajili ya kutambua mchango wa wanawake hawa kwa ujasiri na uthubutu katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.
Hafla hiyo pia itahudhuriwa na Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump ambaye atakuwa ndio mgeni rasmi.
Anna Henga ni moja ya wanawake ambaye juhudi zake katika utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania ni zenye kupigiwa mfano. Wanawake wengine tisa watakaotunukiwa tuzo hiyo wanatoka katika mataifa yafuatayo; Bangladesh, Burma, Djibouti, Egypt, Jordan, Ireland, Montenegro, Peru na Sri Lanka.
Hafla hiyo itaweza kuonekana mubashara kupitia tovuti ya ikulu ya Marekani www.state.gov.
Kadhalika itakuwa moja kwa moja kupitia mtandao wa Twitter@humanrightstz na @StateDept, #WomenofCourage na #MwanamkeJasiri
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.